WINGA mahiri wa kimataifa wa Ivory Coast, Salomon Kalou amesema yuko tayari kuanza kwa mara ya kwanza kuitumikia Hertha Berling katika mchezo wa Bundesliga dhidi ya Freiburg baadae leo. Nyota huyo wa zamani wa Chelsea alicheza akitokea benchi katika mchezo wa Jumamopsi iliyopita ambao walichapwa nyumbani mabao 3-1 dhidi ya Mainz. Kalou alikaririwa na gazeti na Bild la nchi hiyo akidai kuwa kwasasa amerejea katika halia yake ya kawaida tayari kwa ajili ya mchezo wa leo huku akitamba kukaribia kuwa fiti kwa asilimia 100. Meneja wa klabu ya Hertha Jos Luhukay hajaondoa uwezekano wa kumuanzisha Kalou lakini amesema nyota huyo anahitaji muda ili aweze kuimarika zaidi. Kalou mwenye umri wa miaka 29 alijiunga na Hertha akitokea timu ya Lille ya Ufaransa kwa kitita cha euri milioni tatu huku akipewa mkataba wa miaka mitatu na klabu hiyo kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili wa kiangazi mwaka huu.
No comments:
Post a Comment