Monday, September 1, 2014

BAYERN WAMPELEKA GREEN KWA MKOPO HUMBURG.

KLABU ya Bayern Munich imethibitisha kuwa chipukizi Julian Green ameondoka katika timu hiyo na kuhamia Hamburg kwa mkopo wa mwaka mmoja. Humburg wamekuwa katika pilikapilika za kuimarisha kikosi chao kabla ya kufuingwa kwa dirtisha la usajili kufuatia kuanza vibaya msimu wa 2014-2015 na sasa wamemchukua kinda huyo mwenye umri wa miaka 19 katika siku ya mwisho ya usajili. Green amekulia katika shule ya vipaji ya Bayern kabla ya kuibuka katika kikosi cha kwanza katika mchezo dhidi ya CSKA Moscow wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Novemba mwaka jana. Nyota huyo wa kimataifa wa Marekani ambaye alifunga bao moja katika michuano ya Kombe la Dunia nchini Brazil, alikuwa katika hatihati ya kupata muda wa kucheza wa kutosha akiwa Bayern ndio maana amepelekwa kwa mkopo ili aweze kuongeza uzoefu zaidi.

No comments:

Post a Comment