Monday, September 1, 2014

BAADA YA KUSHINDWA KUMSHAWISHI PELLEGRINI, RICHARDS AAMUA KUTIMKIA FIORENTINA.

BEKI wa klabu ya Manchester City, Micah Richards anatyarajiwa kujiunga na klabu ya Fiorentina ya Italia baada ya kumaliza miaka 12 akiwa Etihad. Richards mwenye umri wa miaka 26 tayari ameshawasili Italia na anatarajiwa kuwa Mwingereza wa 24 kuichezea klabu hiyo mara atakapokamilisha usjaili huo. Beki huyo alikuwa mchezaji muhimu ya kikosi cha City kilichonyakuwa taji la Ligi Kuu mwaka 2012 lakini amejikuta akikosa nafasi ya kucheza chini ya meneja Manuel Pellegrini. City pia bado wanasiliza ofa kwa wachezaji wao Matija Nastastic, John Guidetti na Scott Sinclair ambao wanaonekana kutokuwepo katika mipango ya Pellegrini. Richards ambaye ni mzaliwa wa Birmigham alifanikiwa kucheza mechi mbili pekee za Ligi Kuu msimu uliopita na alikuwa amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake.


No comments:

Post a Comment