Monday, September 1, 2014

MANCHESTER UNITED YAZIPIGA BAO ARSENAL NA CITY, YAMNASA FALCAO KWA MKOPO.

KLABU ya Manchester United imekubali kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Colombia, Radamel Falcao kwa mkopo kutoka klabu ya Monaco ya Ufaransa. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 amekuwa akihusishwa na tetesi za kuondoka muda mrefu kiangazi hiki kutoka Monaco ambao walimsajili kwa paundi milioni 50 mwaka jana. Toka ametua Monaco Falcao amefanikiwa kufunga mabao 11 katika mechi 20 huku akikaa nje nusu msimu kutokana na majeruhi ya goti yaliyomsababisha pia kuikosa michuano ya Kombe la Dunia. Mahasimu wa United katika Ligi Kuu Manchester City walishindwa kumuwania nyota huyo kwasababu hawakuweza kumhakikishia namba katika kikosi chao. Falcao pia alikuwa akihusishwa na tetesi za kuwindwa na Arsenal, mabingwa wa Italia Juventus na mabingwa wa Ulaya Real Madrid.

No comments:

Post a Comment