Monday, September 1, 2014

FALCAO AMKIMBIZA HERNANDEZ AAMUA KUTIMKIA MADRID KWA MKOPO.

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Manchester United, Javier Hernandez amejiunga na mabingwa wa Ulaya Real Madrid kwa mkopo wa msimu mmoja. Madrid wanawajibika kumnunua moja kwa moja nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 ambaye alijiunga na United akitokeo Guadalajara mwaka 2010, mara mkopo wake utakapomalizika. United imelazimika kumtoa mshambuliaji huyo kwa mkopo baada ya kukamilisha usajili wa mkopo wa mshambuliaji wa kimataifa wa Colombia Radamel Falcao kutoka Monaco. Hernandez atakluwa mbadala wa mshambuliaji chaguo la kwanza wa Madrid Karim Benzema katika muda wote atakaokuwepo Santiago Bernabeu. Nyota huyo wa kimataifa wa Mexico aliisaidia nchi yake kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Dunia nchini Brazil alkifunga bao katika mchezo wa makundi dhidi ya Croatia.

No comments:

Post a Comment