Thursday, September 25, 2014

CAF CHAMPIONS LEAGUE 2014: SETIF, VITA KUVUNJA MWIKO?

KLABU za Entente Setif ya Algeria na Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC mwishoni mwa wiki hii zinaweza kuandika historia mpya katika mechi zao za nusu fainali za mkondo wa pili wa michuano ya Mataifa ya Afrika. Setif na Vita zilitengenezea ushindi wa mabao 2-1 katika mechi zao za nyumbani dhidi ya TP Mazembe ya DRC na CS Sfaxien ya Tunisia. Lakini katika historia ya miaka 49 ya mashindano hayo katika timu saba ambazo zilijitengenezea ushindi kama huo katika mechi ya kwanza ya nusu fainali hazikufanikiwa kutinga fainali. Klabu ambacho zimewahi kutangulia na ushindi kama huo lakini baadae kushindwa kumaliza kazi walioanza ni pamoja na ASEC Mimosas ya Ivory Coast, Lome 1 ya Togo, Diaraf na Jeanne d’Arc zote za Senegal, Canon Younde ya Cameroon, El-Hilal ya Sudan na Al-Ahly ya Misri.

No comments:

Post a Comment