Thursday, September 25, 2014

ODIMWINGIE APIGWA KISU.

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Stoke City, Peter Odimwingie amethibitisha kuwa upasuaji wake wa goti aliofanyiwa umekuwa wa mafanikio. Mshambualiji huyo wa kimataifa wa Nigeria alipata majeruhi hayo Agosti 30 wakati Stoke ilipoitandika Manchester City bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu uliofanyika katika Uwanja wa Etihad. Odemwingie alithibitisha taarifa hizo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter huku pia akikipongeza kikosi chao kwa kutinga mzunguko wa nne wa michuano ya Kombe la Ligi. Nyota huyo ambaye hatarajii kurejea uwanjani kwa mwaka huu anaamini Stoke inaweza kuendelea kufanya vyema bila uwepo wake.

No comments:

Post a Comment