Thursday, September 25, 2014

NEYMAR ANANIKUMBUSHA ALIVYOKUWA ROMARIO - DUNGA.

KOCHA wa timu ya taifa ya Brazil, Dunga amesema Neymar anamkumbusha jinsi alivyokuwa mshambuliaji nguli Romario na kudai kuwa atakuwa mfano wa kuigwa katika soka duniani. Nyota huyo wa klabu ya Barcelona ameanza vyema msimu huu kwa kufunga mabao matatu katika mechi nne za ligi baada ya kuifungia pia Brazil mabao manne katika Kombe la Dunia kabla ya kuumia mgongo katika robo fainali na kumfanya kutocheza tena michuano hiyo. Dunga amemfananisha Neymar na nyota mwingine wa zamani wa Barcelona na Brazil Romario ambaye amewahi kufanya naye kazi na kudai kuwa kama ilivyo kwa nguli huyo, Neymar naye anafanya kama aliyowahi kufanya wakati akicheza. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa Neymar ni kiongozi wa ufundi na pia ni mfano wa kuigwa nchini Brazil na dunia kwa ujumla jambo ambalo ndiovyo ilivyokuwa kwa Romario enzi zake. Dunga pia alidokeza uwezekano wa kumuita kiungo Kaka katika kikosi chake kama akiendelea kucheza kwa kiwango cha juu kama hivi sasa katika klabu yake ya Sao Paulo.

No comments:

Post a Comment