MICHUANO ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya hatua ya makundi inatarajiwa kuendelea tena kesho na keshokutwa ambapo viwanja mbalimbali vinatarajiwa kuwaka moto. Katika michezo ya kesho macho yatakuwa yameelekezwa kwa matajiri na mabingwa wa soka nchini Uingereza Manchester City ambao watakuwa wenyeji wa AS Roma ya Italia katika mchezo wa kundi E utakaofanyika katika Uwanja wa Etihad. City wataingia katika mchezo wakihitaji ushindi baada ya kupoteza mchezo wao kwanza waliochezwa na mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich ambao walifungwa bao 1-0 huko Allianz Arena. Katika mchezo mwingine wa kundi hilo CSKA Moscow ya Urusi watakuwa nyumbani kujiuliza mbele ya Bayern baada ya kuchabangwa mabao 5-1 na Roma katika mchezo wao uliopita. Kwa upande wa Kundi F matajiri wa Ufaransa, Paris Saint-Germain,PSG watakuwa wenyeji wa Barcelona wakitafuta alama tatu muhimu baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Ajax Amsterdam ya Uholanzi. Barcelona wao walipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 katika mchezo dhidi ya APOEL Nicosia ya Cyprus ambao kesho watakuwa wenyeji wa Ajax katika mchezo mwingine wa kundi hilo. Katika mechi zao za kwanza Barcelona ambao ndio wanaongoza kundi hilo walipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya timu ya APOEL Nicosia ya Cyprus huku PSG wao wakitoa sare ya bao 1-1 dhidi ya Ajax Amsterdam ya Uholanzi. Mchezo mwingine utakaovuta hisia za mashabiki hapo kesho ni wa kundi G ambao utawakutanisha vinara wa Ligi Kuu Chelsea wakaokuwa wageni wa Sporting Lisbon ya Ureno huku Schalke ya Ujerumani wakiwa wenyeji wa NK Maribor ya Slovenia timu zote katika kundi hili zilitoka sare ya bao 1-1 katika mechi zao za kwanza. Kesho pia kutakuwa na michezo itakayochezwa katika kundi H ambapo BATE Borislov ya Belarus watawakariisha Athletic Bilbao ya Hispania na Shakhtar Donetsk ya Ukraine wakiwa wenyeji wa FC Porto ya Ureno.
No comments:
Post a Comment