WACHEZAJI 26 wameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa Tanzania,Taifa Stars kwa ajili mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Benin itakayochezwa Oktoba 12 mwaka huu jijini Dar es Salaam. Kocha wa Stars Mart Nooij ambaye yuko jijini Cairo, Misri kwenye kongamano la makocha la Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika-CAF, amesema kikosi cha Taifa Stars kitaingia kambini Oktoba 6 mwaka huu jijini Dar es Salaam. Wachezaji walioitwa na vilabu wanavyotoka ni makipa Deogratias Munishi,(Yanga), Aishi Manula na Mwadini Ali wote Azam. Mabeki ni Said Moradi, Azam, Shomari Kapombe (Azam), Oscar Joshua (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Aggrey Morris (Azam), Miraji Adam (Simba), Charles Edward (Yanga) na Emmanuel Simwanda (African Lyon). Viungo ni Erasto Nyoni (Azam), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar), Amri Kiemba (Simba), Himid Mao (Azam), Salum Abubakar (Azam), Said Ndemla (Simba) na Haruna Chanongo (Simba). Washambuliaji ni Khamis Mcha (Azam), Simon Msuva (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DR Congo), Mbwana Samata (TP Mazembe, DR Congo), Mrisho Ngasa (Yanga), Mwegane Yeya (Mbeya City), na Juma Liuzio (Zesco, Zambia).
No comments:
Post a Comment