Tuesday, September 30, 2014

NTAONDOKA CHELSEA NIKIFUKUZWA - MOURINHO.

MENEJA wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho amesisitiza kuwa ataondoka katika timu hiyo endapo kama atatimuliwa. Mara ya kwanza Mourinho kuondoka Stamford Bridge ilikuwa Septemba mwaka 2007 baada ya kushindwa kuelewana na mmiliki wa klabu hiyo Roman Abramovic. Kocha huyo raia wa Ureno aliondoka na kwenda kupata mafanmikio nchini Italia na Hispania akiwa na Inter Milan na Real M,adrid lakini aliwashangaza wengi kwa kurejea tena Chelsea katika kipindi cha kiangazi mwaka jana kufuatia kuondoka kwa Rafa Benitez. Katika kipindi hicho ilikuwa imeripotiwa kuwa Mourinho atarejea nchini Uingereza kuchukua nafasi ya Sir Alex Ferguson kama meneja wa Manchester United lakini kocha huyo badala yake akamchukua David Moyes kushika nafasi yake. Mourinho amesema ana mpango wa kukaa muda mrefu Chelsea lakini kama itatokea kutimuliwa anaweza kufikiria kutafuta timu nyingine ya Ligi Kuu.

No comments:

Post a Comment