Thursday, October 2, 2014

TULISTAHILI KUFUNGWA - GERRARD.

NAHODHA wa klabu ya Liverpool, Steven Gerrard amehoji shauku na dhamira ya wachezaji wenzake baada ya kutandikwa bao 1-0 na FC Basel katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya. Gerrard amesema hakustahili kupata chochote katika mchezo huo kwani walicheza kizembe huku wakirudia makosa ya mara ya kwanza kwa kushindwa kuokoa vyema mipira langoni mwao. Matokeo hayo sasa yanaishusha Liverpool mpaka katika nafasi ya tatu katika kundi B huku wakikabiliwa na mchezo dhidi ya mabingwa watetezi Real Madrid katika mechi zao mbili zijazo. Gerrard amesema Basel walicheza vyema huku wakionyesha uchu wa kupata ushindi kuanzia mwanzo mpaka mwisho tofauti na wao ambao walionekana kama bado hawajazinduka.

No comments:

Post a Comment