Thursday, October 2, 2014

SINA MPANGO WA KUSHINDANA NA RONALDO - MESSI.

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi amesisitiza kuwa hana nia ya kushindana na Cristiano Ronaldo kwa ajili ya tuzo ya mchezaji bora wa dunia. Kushinda tuzo sita za Ballon d’Or kati yao, wawili hao wamekuwa wakifananishwa mara nyingi na wachezaji wenzao, wachambuzi na hata mashabiki. Hata hivyo Messi amesisitiza kuwa huwa hafuatilii sana mambo ya mashindano baina yao kwani kikubwa kinachomsukuma kufanya vyema sio tuzo binafsi bali ni mataji kwa ajili ya klabu yake. Messi amesema hana haja ya kushindana na Ronaldo kwani nia na madhumuni yake makubwa na kuisadia timu yake kushinda mataji mechi iwezekanavyo.

No comments:

Post a Comment