KLABU ya Manchester United inajipanga kutoa ofa ya kitita cha euro milioni 13 kwa ajili ya kumnasa kiungo wa Real Madrid Sami Khedira katika dirisha dogo la usajili Januari mwakani. United imemua kuhamishia nguvu zao kwa kiungo huyo wa kimataifa wa Ujerumani baada ya kuhabalishwa kuwa kiungo wa AS Roma Kevin Strooman aliyekuwa akiwindwa na Louis van Gaal hataweza kuondoka katika kipindi hicho. Van Gaal ameruhusiwa kutumia tena fedha katika usajili wa Januari ili kuendelea kuimarisha kikosi cha United baada ya kusajiliwa kwa Angel Di Maria, Ander Herrera na Radamel Falcao katika majira ya kiangazi. Inafahamika kuwa Khedira yuko tayari kuondoka na kwenda katika timu inayoshiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya lakini United wao wameonyesha wako tayari kumlipa mshahara wa paundi 255,000 kwa wiki anaouhitaji ili atue Old Trafford. Katika kipindi cha kiangazi Khedira aliwekwa sokoni kwa kitita cha euro milioni 26 na kulikuwa na tetesi za Arsenal kumuhitaji lakini walishindwana kutokana na kiasi kikubwa cha mshahara alichohitaji.
No comments:
Post a Comment