Thursday, September 25, 2014

DAKTARI ATHIBITISHA MUSANA ALIKUFA KWA BRONCOPNEUMONIA.

RIPOTI ya daktari aliyefanyia uchunguzi mwili wa mchezaji wa klabu ya Simba Fahad Musana imedai kuwa mchezaji huyo alifariki duniani kutokana na kusumbuliwa na tatizo la kupumua kwa kitaalamu bronchopneumonia. Taarifa hiyo iliwasilishwa na meneja wa klabu hiyo Perez Muwezi juzi wakati wa mazishi ya mchezaji huyo katika kijiji cha Walugogo, wilaya ya Iganga nchini Uganda. Taarifa hiyo ilitolewa kutoka hospitali ya rufaa ya taifa ya Mulago na kusainiwa na daktari aliyefanya uchunguzi huo Acola Caroh. Musana alifariki dunia Jumapili iliyopita wakati akiangalia mchezo wa Ligi Kuu nchini Uingereza kati ya Chelsea na Manchester City huko Bombo ambapo ndipo maskani ya klabu yake ya Simba.

No comments:

Post a Comment