Thursday, September 25, 2014

FIFA YATUPILIA MBALI RUFANI YA SANTOS.

SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limetupilia mbali rufani ya kocha mpya wa timu ya taifa ya Ureno Fernando Santos aliyokuwa kipinga kufungiwa mechi nane kutokana na makosa ya utovu wa nidhamu katika michuano ya Kombe la Dunia. FIFA imedai katika taaifa yake kuwa kamati yake ya rufani imekataa uitetezi wa kocha huyo wa zamani wa Ugiriki. Santos sasa aneweza kukata tena rufani katika Mahakama Kimataifa ya Michezo-CAS. Kocha huyo aliajiriwa na Shirikisho la Soka la Ureno Juzi pamoja na kuwa amefungiwa kukaa katika benchi la ufundi kwa mechi nane. Santos ataanza kutumikia adhabu yake hiyo wakati wa mechi za kufuzu michuano ya Ulaya ingawa ameruhusiwa kuchagua mechi na kuhudhuria vipindi vya mazoezi. Santos mwenye umri wa miaka 59, aliwatukana waamuzi wakati Ugiriki ilipotolewa na Costa Rica katika hatua ya timu 16 bora katika michuano hiyo iliyofanyika nchini Brazil.

No comments:

Post a Comment