Thursday, September 25, 2014

KOMBE LA LIGI: LIVERPOOL KUIVAA SWANSEA, MAN CITY NA NEWCASTLE, CHELSEA WAPEWA VIBONDE KUTOKA DARAJA LA NNE.

MENEJA wa klabu ya Liverpool, Brendan Rodgers anatarajia kukwaana na klabu yake ya zamani ya Swansea City katika mzunguko wa nne wa michuano ya Kombe la Ligi kufuatia ratiba iliyopangwa jana. Liverpool ambao walitinga hatua hiyo baada ya kuitoa Middlesbrough kwa changamoto ya mikwaju ya penati 14-13, watakuwa wenyeji wa Swansea ambao kwasasa wanashika nafasi ya tano katika msimamo wa Ligi Kuu. Mabingwa watetezi wa michuano hiyo Manchester City wao watakuwa wenyeji wa Newcastle United na vinara wa Ligi Kuu Chelsea watasafiri kuifuata timu ya daraja la nne ya Shrewsbury Town ambayo ni timu ya daraja la chini zaidi kubakia katika michuano hiyo. Mechi nyingine Stoke City wao watakuwa wenyeji wa Southampton huku Tottenham Hotspurs nao wakiikaribisha timu ya daraja la pili Brighton & Hove Albion. Wengine ni West Bromwich Albion ambao watakuwa wageni wa timu ya daraja la pili Bournemouth, MK Dons watachuana na wenzao wa daraja la tatu Sheffield United huku Fulham nao wakiwakaribisha wenzao wa daraja la pili Derby County.

No comments:

Post a Comment