KOCHA mpya wa timu ya taifa ya Brazil, Dunga amemuita mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya Real Madrid, Manchester City na AC Milan, Robinho kuziba pengo la majeruhi Hulk kwa ajili ya mechi mbili za kimataifa za kirafiki dhidi ya Colombia na Ecuador. Dunga ambaye alitaja kikosi chake cha kwanza toka achukue mikoba kwa mara ya pili kutoka kwa Luiz Felipe Scolari baada ya Kombe la Dunia, amemchukua nyota huyo mwenye umri wa miaka 30 ambaye ameichezea nchi hiyo mechi 92. Robinho amerejea nyumbani Brazil kucheza katika klabu ya Santos ambayo ndio alianzia kucheza soka lake baada ya AC Milan kumuuza kwa mkopo wa mwaka mmoja. Dunga ambaye aliwahi kuinoa Brazil katika miochuano ya Kombe la Dunia mwaka 2010 kabla ya kutimuliwa sasa anaelekea katika mchezo dhidi ya Colombia utakaochezwa jijini Miami Ijumaa hii akiwa na wachezaji 10 pekee waliokuwepo katika kikosi cha Scolari. Baada ya kukwaana na Colombia, Brazil itachuana na Ecuador huko East Rutherford jijini New Jersey Septemba 9 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment