Monday, September 1, 2014

PIRLO BADO ANA UWEZO WA KUVAA JEZI YA ITALIA - CONTE.

KOCHA mpya wa timu ya taifa ya Italia, Antonio Conte amesema Andrea Pirlo anaweza kuvaa tena jezi ya nchi hiyo pamoja na kupendekeza baada ya Kombe la Dunia kuwa atawapisha vijana wanaochipukia. Conte amesema anataka kuwa na uhakika kama atakuwa katika kiwango kile kile kwasababu anamfahamu ni mpambanaji na amemuhakikishia anapatikana kama atamuhitaji katika kikosi chake. Kwasasa Pirlo yuko nje ya uwanja mpaka Octoba akiuguza majeruhi ya paja hivyo kumaanisha kuwa atakosa mchezo wa kirafiki wa kimataifa wa dhidi ya Uholanzi utakaochezwa Ijumaa hii huko Bari na pia mchezo wa kufuzu michuano ya Ulaya mwakani dhidi ya Norway jijini Oslo Jumanne ijayo. Conte amemfundisha Pirlo akiwa Juventus kwa miaka mitatu ambapo wamefanikiwa kushinda taji la Serie katika kila mwaka kabla ya kuamua kuchukua mikoba ya timu ya taifa kutoka Cesare Prandelli. Pamoja na kumzungumzia Pirlo, Conte alikataa kutoa sababu za kuamua kumucha mshambuliaji mpya wa Liverpool Mario Balotelli katika kikosi chake.

No comments:

Post a Comment