SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA sasa limeipa Nigeria muda wa mpaka Septemba 8 kwa kiongozi wa Shirikisho la Soka la nchini hiyo-NFF Chris Giwa awe amejiuzulu au wafungiwe. Katika barua yake iliyotumwa kwa katibu mkuu wa NFF Musa Amadu, FIFA wameeleza kuwa kamati yake ya dharura imeamua kuisimamisha nchi hiyo mpaka mtajwa atapoachia madaraka na katibu mkuu aweze kuendelea na majukumu yake bila kubugudhiwa. FIFA pia ilifafanua kuwa kamati ya utendaji NFF iliyoteuliwa Agosti 25 mwaka huu ikiwa chini ya rais Aminu Maigari itatakiwa kuitisha mkutano mkuu haraka ili kuchagua wajumbe wa kamati ya uchaguzi kabla ya kuitisha mkutano mwingine wa uchaguzi kwa ajili ya viongozi wapya wa shirikisho hilo. FIFA imeweka wazi katika barua yake hiyop iliyosainiwa na kamtibu mkuu wake Jerome Valcke kuwa mara NFF itakapofungiwa nchi hiyo haitapata nafasi ya kushiriki michuano yoyote ya kimataifa ikiwemo hata ile ya kirafiki. Hata hivyo uamuzi huo wa FIFA kusogeza mbele muda huo umetoa ahaueni kwa mchezo wao wa kufuzu Mataifa ya Afrika dhidi ya Congo utakaofanyika Jumamosi hii huko Calabar lakini kuna wasiwasi wa mchezo wao dhidi ya Afrika Kusini unaotarajiwa kufanyika Septemba 10 usifanyike kama maagizo hayo hayatazingatiwa.
No comments:
Post a Comment