KLABU ya Real Madrid imefanikiwa kumnasa beki wa Manchester United Guillermo Varela kwa mkopo wa msimu mzima. Beki huyo mwenye umri wa miaka 21 alikuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na meneja wa zamani David Moyes, lakini hakuwahi kucheza katika kikosi cha kwanza toka atoke Penarol. Varena sasa anatarajiwa kucheza katika kikosi cha pili cha Madrid ambacho kinanolewa na Zinedine Zidane. Beki huyo anakuwa mchezaji wa pili wiki hii kusajiliwa kwa mkopo kwenda Madrid kutokea United baada ya Javier Hernandez naye kuhamia kwa mabingwa hao wa Ulaya.
No comments:
Post a Comment