Wednesday, September 3, 2014

MAJERUHI YAMUONDOA FOSTER KAMBI YA UINGEREZA.

CHAMA cha cha Soka cha Uingereza-FA kimetangaza kuondolewa kwa golikipa Ben Foster katika kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo kitakachocheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Norway baadae leo na mchezao wa kufuzu michuano ya Ulaya mwakani dhidi ya Switzerland wiki ijayo baada ya kupata majeruhi akiwa mazoezini. FA haikufafanua kwa undani majeraha aliyopata lakini vyombo vya habari vimeripoti kuwa golikipa huyo wa klabu ya West Bromwich Albion ameumia kidole gumba. Uingereza itacheza na Norway katika Uwanja wa Wembley kabla ya kusafiri kwenda jijini Basle kwa ajili ya mchezo wao wa kufuzu michuano ya Ulaya Jumatatu. Taarifa ya FA iliongeza kuwa kocha wa Uingereza Roy Hodgson hataita golikipa mwingine kuziba nafasi ya Foster ambaye alikuwa kama mbadala wa kipa namba moja Joe Hart.

No comments:

Post a Comment