WACHEZAJI wa Manchester United wanalazimika kukabidhi simu zao usiku kabla ya mechi chini ya sheria mpya kali kutoka kwa meneja wao Louis van Gaal. Kocha huyo raia wa Uholanzi amekuwa akiweka sheria kadhaa toka achukue mikoba hiyo kutoka kwa David Moyes kiangazi hiki huku pia akimuacha mchezaji yeyote ambaye anachelewa chai ya asubuhi siku ya mchezo. Lakini mpaka sasa mbinu hizo za Van Gaal zimeonyesha kushindwa kubadili matokeo kwani United imeshindwa kupata ushindi wowote katika mechi zake tatu za Ligi walizocheza. Baada ya kufungwa na Swansea City katika mchezo wa ufunguzi na United walitoa sare katika mchezo dhidi ya Sunderland na Burnley kabla ya kutolewa katika Kombe la Ligi kwa kuchabangwa mabao 4-0 na MK Dons.
No comments:
Post a Comment