Wednesday, September 3, 2014

ODEMWINGWE KUFANYIWA UPASUAJI WA GOTI.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Nigeria, Peter Odemwingie amebainisha kuwa sasa anahitaji kufanyiwa upasuaji kutokana na majeraha ya goti aliyonayo. Odemwingie sasa anategemewa kukosa sehemu ya msimu wa Ligi Kuu kufuatia kuumia katika mchezo ambao Stoke City waliitandika Manchester City kwa bao 1-0 Jumamosi iliyopita. Taarifa zinadai kuwa mchezaji huyo anaweza kuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi 10 au zaidi. Odemwingie mwenye umri wa miaka 33 alithibitisha hayo jana katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter kwa kudai kuwa atakosa mechi nyingi za ligi msimu huu. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa atafanya kila naloweza kuhakikisha anarejea tena uwanjani akiwa fiti zaidi na kuendelea kuisaidia timu yake. Majeruhi ya Odemwingie ambaye anachukuliwa kama mchezaji muhimu katika kikosi cha Stoke yamemlazimisha meneja Mark Hughes kumsajili winga wa kimataifa wa Morocco Oussama Assaidi kwa mkopo kutoka Liverpool katika siku ya mwisho kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili majira ya kiangazi.

No comments:

Post a Comment