MENEJA wa timu ya taifa ya Uingereza, Roy Hodgson amesema kikosi chake chenye sura mpya kinaweza kufuta kovu la nchi hiyo kushindwa kutamba katika Kombe la Dunia nchini Brazil. Mshambuliaji Wayne Rooney kwa mara ya kwanza ataingoza nchi hiyo akiwa nahodha mpya wakati watakapochuana na Norway katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika baadae leo. Huo ni mchezo wa kwanza kwa Uingereza toka alipoondolewa katika hatua makundi katika Kombe la Dunia bila kushinda mchezo wowote kati ya mitatu waliyocheza. Viungo wa muda mrefu Frank Lampard na Steven Gerrard wote wametangaza kustaafu soka la kimataifa tpoka Uingereza ilipotolewa katika michuano hiyo baada ya kung’ang’aniwa sare ya bila kufungana na Costa Rica huko Belo Horizonte. Hodgson ameita baadhi ya wachezaji ambao ndio wanaitumikia nchi hiyo kwa mara ya kwanza akiwemo beki wa Arsenal Calum Chambers, beki wa kushoto wa Tottenham Hotspurs danny Rose na kiungo wa Newcastle United Fabian Delph. Kocha huyo amesema ana matumaini makubwa na kikosi hicho kuwa kinaweza kuwasahaulisha matokeo mabovu waliyopata katika Kombe la Dunia na kuwafanya kurejeasha hali ya kujiamini.
No comments:
Post a Comment