Wednesday, September 3, 2014

ILIKUWA NDOTO ZANGU ZA MUDA MREFU KUITUMIKIA ARSENAL - WELBECK.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Uingereza, Danny Welbeck amesema alikuwa akiwaza mwenyewe akiichezea Arsenal wakati bado akiwa Manchester United na amefurahishwa baada ya uhamisho wale kukamilika. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 ametua Arsenal kwa kitita cha paundi milioni 16 katika siku ya mwisho ya usajili wa majira ya kiangazi. Welbeck ambaye kwasasa yupo katika majukumu ya kimataifa na Uingereza, amekuwepo Old Trafford toka akiwa na umri wa miaka nane. Lakini nyota huyo aliuambia mtandao wa Arsenal kuwa amekuwa akifikirtia mwenyewe kuitumikia timu hiyo hivyo jambo kufanikiwa ni jambo ambalo limemfurahisha sana.

No comments:

Post a Comment