KOCHA wa timu ya taifa ya Senegal, Alain Giresse ametangaza kuwa mshambuliaji wa klabu ya Besiktas Demba Ba hatacheza mchezo wa kwanza wa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika dhidi ya Misri Ijumaa hii. Senegal itakuwa mwenyeji wa Misri katika mchezo huo utakaofanyika Septemba 5 jijini Dakar. Ba alikuwa mmoja ya wachezaji walioitwa katika kikosi hicho kabla ya Giresse hajamuondoa kutokana na kupata majeraha akiwa na Besiktas katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Arsenal. Taarifa zinadai kuwa kuna uwezekano mkubwa Ba akaukosa na mchezo wa pili wa kufuzu Afcon dhidi ya Botswana. Misri tayari wameshatua Dakar jana kwa ndege ya kukodi tayari kwa mchezo huo huku wakitarajiwa kurudi nyumbani na kuchezo mchezo wao wa pili dhidi ya Tunisia utakaofanyika jijini Cairo.
No comments:
Post a Comment