NGULI wa soka wa zamani wa Brazil, Zico amekubali kuinoa klabu ya FC Goa katika msimu wa kwanza wa Ligi Kuu nchini India. Zico mwenye umri wa miaka 61 amewahi kuichezea Brazil mechi 71 huku akicheza pia katika fainali za Kombe la Dunia mwaka 1978, 1982 na 1986 huku akiwapia kuzifundisha nchi za Brazil, Japan, Turkey, Urusi, Ugiriki, Iraq na Qatar. Katika taarifa iliyotolewa na uongozi wa wa ligi hiyo mpya ilithibitisha taarifa hizo huku ikidai kuwa Zico alisaini mkataba wake jijini Rio de Janeiro. Taarifa iliendelea kudai kuwa wawakilishi wa klabu hiyo watasafiri kwenda Brazil kwa ajili ya kumsaidia Zico kukamilisha taratibu zake za kibali cha kusafiria kabla ya kwenda India. ISL ina matumaini kuwa umaarufu wa soka utaongezeka nchini India kutokana na michuano hiyo itakayochukua wiki 10, huku ikitarajiwa kuanza Octoba mwaka huu.
No comments:
Post a Comment