Wednesday, September 3, 2014

NDOTO ZANGU ZIMETIMIA - FALCAO.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Colombia, Radamel Falcao amesema kuwa ametimiza ndoto zake baada ya kukamalisha usajili wa mkopo kwenda Manchester United akitokea Porto juzi usiku. Falcao aliiambia luninga ya klabu hiyo MUTV kuwa alikuwa na ndoto za siku nyingi kukipiga katika Ligi Kuu nchini Uingereza kutokana na ushindani uliopo. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa ametua katika klabu ambayo ni bora kabisa nchini humo na sasa kila kitu kinakwenda sawa. Falcao mwenye umri wa miaka 28 alisafiri kwenda jijini Manchester kwa ajili ya vipimo vya afya Jumatatu jioni huku United wakithibitisha dili hilo baada ya kupita saa mbili na nusu toka dirisha la usajili lifungwe. United wameilipa Monaco kitita cha paundi milioni sita ili kupata huduma ya Falcao kwa msimu mmoja huku wakiwa na chaguo la kumsajili moja kwa moja wakitoa kitita kingine cha euro milioni 55.

No comments:

Post a Comment