KIUNGO wa kimataifa wa Nigeria, John Mikel Obi ameamua kuchukua tahadhari kufuatia kulipuka kwa ugonjwa wa Ebola katika baadhi ya sehemu nchini humo. Nyota huyo anayekipiga katika klabu ya Chelsea aliwasili mjini Calabar tayari kwa ajili ya mchezo wa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika dhidi ya Congo Jumanne ijayo akiwa na amevaa kinga mikononi mwake huku akiwapasha waliokuwa wakimshangaa kuwa anachukua tahari kabla ya hatari. Msemaji wa timu ya taifa ya Nigeria maarufu kama Super Eagles, Ben Alaiya ambaye alithibitisha taarifa hizo amesema wachezaji wenzake na Obi Mikel wameona kama jambo la kuchekesha kwa mambo anayofanya kioungo huiyo. Alaiya amesema kambini kila kitu kiko shwari lakini kumekuwa na utani unaoendelea kuhusu tukio la Obi Mikel kuja na kinga nyingi za mikono kama tahadhari ya kujikinga na Ebola. Hata hivyo, Alaiya amesema pamoja na kwamba hakuna mgonjwa yeyote aliyepatikana katika mji wa Calabar lakini wamechukua tahadhari kadhaa ili kuhakikisha wachezaji wote wanakuwa salama muda wote watakaokuwepo hapo.
No comments:
Post a Comment