MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger anaamini kuwa timu hiyo haina bahati kutokana na idadi ya mabeki wake waliokuwa majeruhi na kusisitiza kusajili wachezaji wa kuziba nafasi hizo katika usajili wa majira ya kiangazi ilikuwa kazi ngumu. Kuondoka kwa Thomas Vermaelen kwenda Barcelona kwa kitita cha euro milioni 19, kujumuisha na kushindwa kusajiliwa kwa beki wa kimataifa wa Ugiriki Kostas Manolas kumeifanya Arsenal kuanza msimu wakiwa na wachezaji sita pekee katika nafasi za ulinzi kati ya nne zilizopo. Kwasasa Arsenal wana majeruhi Mathieu Debuchy ambaye atakuwa nje kwa miezi mitatu wakati Ncho Monreal naye yuko nje kutokana na matatizo ya mgongo kumeifanya timu hiyo kuonyesha udhaifu mkubwa katika safu hiyo. Wenger amekiri kua matatizo ya majeruhi yamewasababishia matatizo mwanzoni mwa msimu huu lakini amedai alifanya kila analoweza kujaribu kusajili mabeki zaidi katika wakati wa kiangazi. Arsenal ilitumia zaidi ya euro milioni 888 kwa ajili ya kuwasajili Alexis Sanchez, Danny Welbeck, Calum Chambers, Debuchy na David Ospina katika majira haya ya kiangazi.
No comments:
Post a Comment