Friday, September 26, 2014

DEBRY ZA LIGI KUU MWISHONI MWA WIKI.

MWISHONI mwa wiki katika michezo ya Ligi Kuu nchini Uingereza tutashuhudia mechi mbili zitakazowahutanisha mahasimu katika miji wanayotoka. Kwa upande wa kaskazini mwa jiji la London Arsenal watawakaribisha majirani zao Tottenham Hotspurs wakati Liverpool wao watakuwa wenyeji wa majirani zao wa Merseyside timu ya Everton. Mechi hizo ambazo zitapigwa kesho zinaleta mvuto wa ziada kwani zote nne zinahitaji ushindi baada ya kuanza kwa kusuasua toka msimu ulipoanza. Liverpool ambao walipoteza taji kwa tofauti ya alama chache mbele ya Manchester City msimu uliopita na Everton kumaliza katika nafasi ya tano wakiweka rekodi kwa kukusanya alama nyingi zaidi, kwasasa wote wako chini katika nafasi ya 11 na 14 kuelekea katika mchezo wao huo. Kwa upande wa Arsenal wao kwasasa wanashika nafasi ya nne wakiwa wamejikusanyia alama tisa katika mechi tano walizocheza huku mahasimu wao Spurs wakiwa nafasi ya tisa kwa kujikusanyia alama saba.

No comments:

Post a Comment