BONDIA mahiri wa Marekani, Floyd Mayweather amemdhihaki bondia mahiri wa Uingereza Amir Khan katika mkutano wake na wanahabari lakini amekubali kuwa anaweza kupigana na bondia huyo katika mapambano yake yajayo. Baada ya Mayweather kumchakaza Marcos Maidana wa Argentina katika pambano lililofanyika Jumamosi usiku jijini Las Vegas, hatimaye sasa anaweza kukutana na Manny Pacquiao katika pambano lake litakalofuata.
Amir Khan akiwa na Mike "Iron" Tyson katika pambano la Mayweather mwishoni mwa wiki iliyopita. |
Lakini Mayweather amekiri kuwa pambano dhidi ya Khan katika Uwanja wa Wembley linawezekana pamoja na kuponda rekodi za mapambano yake yaliyopita. Pamoja na kumsifia Khan kama bondia mzuri ana mwenye ushindani lakini Mayweather ambaye hajawahi kupigwa katika mapambano 47 ya ngumi za kulipwa aliyopigana alimdhihaki kwa kudai kuwa amekuwa bingwa kwa kipindi kirefu wakati ambapo toka bondia huyo amekuwa akicheza ngumi za ridhaa.
No comments:
Post a Comment