Monday, September 15, 2014

PISTORIOUS HATIHATI KUALIKWA MASHINDANO YA DIAMOND LEAGUE.

MWANARIADHA mlemavu wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius anaweza asiruhusiwe kushiriki mashindano ya Diamond League siku zijazo kwa mujibu ya waratibu wa mashindano hayo. Pistorius alikutwa na hatia ya kuua bila kukusudia baada ya jaji kuamua kuwa alimuua mpenzi wake Reeva Steenkamp kwa makosa. Nyota huyo anaweza kukabiliwa na kifungo cha miaka 15 jela ingawa jaji anaweza kubadilisha kifungo hicho kwa kumtoza faini hivyo kumruhusu kuendelea kushindana tena. Akihojiwa kama ataweza kumualika Pistorius katika mashindano ya Diamond League ya Brussels ofisa mkuu Wilfried Meert amesema suala hilo halitawezekana. Meert anaamini msimamo wake juu ya Pistorius ambaye ni mshindi wa medali sita za dhahabu katika michuano ya paralimpiki utaungwa mkopo na waratibu wengine wa mashindano. Pistorius anatarajiwa kuhumiwa rasmi Octoba 13 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment