Monday, September 15, 2014

CORINTHIANS YAWAANGUKIA MASHABIKI WAKE WATUKUTU.

KLABU ya Corinthians ya Brazil imewaangukia mashabiki wake na kuwaomba kutopiga kelele za matusi wakati wa mchezo wao dhidi ya mahasimu wao Sao Paulo. Mashabiki wa soka nchini Brazil wamekuwa wakimlenga golikipa wa Sao Paulo ambao watacheza nao Septemba 21 mwaka huu, kwa kukebehi tabia yake ya ushoga wakati akipiga mipira ya adhabu. Mapema mwezi huu Shirikisho la Soka nchini Brazil liliiondoa klabu ya Gremio kushiriki michuano ya Kombe la Brazil kwasababu kelele za unyanyasaji wa kibaguzi zilizokuwa zikitolewa na mashabiki wake. Shirikisho hilo limedai kuwa halitavumilia tena lugha za unyanyasaji viwanjani. Ili kuepukana na adhabu kama hiyo klabu hiyo imetoa ilani kwa mashabiki wake kukoma kutumia lugha za kibaguzi sambamba na zile za unyanyasaji.

No comments:

Post a Comment