MENEJA wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho amemtupia lawama Cristiano Ronaldo kwa kushindwa kwake kunyakuwa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati akiinoa Real Madrid. Mourinho alijiunga na na Madrid mwaka 2010 baada ya kuisaidia Inter Milan kunyakuw ataji hilo lakini katika msimu mitatu aliyokuwa Santiago bernabeu alishindwa kabisa kupata mafanikio barani Ulaya akiwa ameambulia kuingoza timu hiyo mpaka hatua ya nusu fainali katika kipindi chote hicho. Mara ya mwisho Mourinho kukaribia kutinga fainali ya michuano ya hiyo ilikuwa msimu wa mwaka 2011-2012 wakati walipokwenda katika hatua ya changamoto ya mikwaju ya penati baada ya muda wa nyongeza katika nusu fainali ya pili lakini walitolewa baada ya nyota wake akiwemo Ronaldo, Kaka na Sergio Ramos kukosa penati muhimu. Akihojiwa Mourinho ametamba kuwa kushinda taji la michuano hiyo mara mbili kama imefanya kazi yake hiyo kuwa ya kipekee. Mourinho amesema amekuwepo katika nusu fainali kadhaa na baadhi imekuwa ngumu kukubali kushindwa kama goli walilofungwa na Liverpool wakati akiwa na Chelsea mwaka 2005 pamoja matuta ya mwaka 2011 wakati mchezaji wao tegemeo Ronaldo alipokosa penati ya kwanza.
No comments:
Post a Comment