LIGI kuu nchini Uingereza inaendelea tena leo ambapo kutakuwa na mchezo mmoja utakaozikutanisha timu za Hull City na West Ham United katika Uwanja wa Kingston Communication-KC. Hull wataingia katika mchezo huo bila ya kuwa na mshambuliaji wao tegemeo Abel Mathias Hernandez Platero. Nyota huyo wa kimataifa wa Uruguay mwenye umri wa miaka 24 alisajiliwa na Hull katika siku ya mwisho ya usajili akitokea klabu ya Palermo lakini mashabiki watalazimika kusubiri kutokana na mchezaji huyo kuchelewa kupata kibali cha kufanya kazi Uingereza. Hata hivyo kocha wa Hull Steve Bruce atapata ahueni baada ya kuwepo mshambuliaji mwingine wa kimataifa wa Uruguay Gaston Ezequiel Ramirez Pereyra.
No comments:
Post a Comment