Monday, September 15, 2014

MAREKANI YATETEA UBINGWA WAO WA KOMBE LA DUNIA LA MPIRA WA KIKAPU.

TIMU ya taifa ya mpira wa kikapu ya Marekani maarufu kama Dream Team imefanikiwa kutetea ubingwa wa wake wa michuano ya Kombe la Dunia la mchezo huo iliyomalizika nchini Hispania jana usiku. Marekani walifanikiwa kuondoka na taji hilo walilonyakuwa mwaka 2010 nchini Uturuki baada ya kuitandika Serbia kwa vikapu 129-92. Hii inakuwa michuano ya 17 toka ibadilishwe na kuwa Kombe la Dunia baada ya mara ya kwanza kuitwa mashindano ya ubingwa wa mpira wa kikapu. Michuano ya mwaka huu itakuwa ya mwisho kufanyika katika mzunguko wa miaka minne kwani michuano itakayokuja itafanyika baada ya miaka mitano yaani mwaka 2019 ili kurekebisha hesabu za miaka kuingiliana na ratiba ya Kombe la Dunia la FIFA.

No comments:

Post a Comment