MENEJA wa klabu ya Manchester United, Louis van Gaal ameanza kutamba kuwa anataka kulirejesha taji la Ligi Kuu Old Trafford. Kauli ya kocha huyo Mholanzi imekuja kufuatia ushindi mnono wa mabao 4-0 waliopata dhidi ya Queens Park Rangers jana ukiwa ni ushindi wake wa kwanza toka achukue mikoba ya kuinoa klabu hiyo katika kipindi cha majira ya kiangazi. Akihojiwa mara baada ya mchwezo huo, Van Gaal amesema anataka kushinda taji la Ligi Kuu kama sio msimu huu basi msimu unakuja au unaofuata lakini anataka kuwapa furaha mashabiki wa klabu hiyo. Van Gaal ambaye amewahi kushinda mataji ya ligi katika msimu wake wa kwanza wakati akizinoa Barcelona na Bayern Munich, amewekewa malengo ya kumaliza katika nafasi tatu za juu msimuu na Ofisa Mkuu Ed Woodward. Baada ya kufunga mabao mawili katika mechi nne zilizopita chini ya Van Gaal, United jana walionyesha mchezo mzuri dhidi ya QPR ambapo mabao yake yalifungwa na Angel Di Maria, Ander Herrera, Wayne Rooney na Juan Mata.
No comments:
Post a Comment