Saturday, September 13, 2014

ARSENAL YATOKA SARE NA CITY.

BAO la kusawazisha katika dakika za mwisho kutoka kwa Martin Demichelis lilitosha kuipa Manchester City sare ya mabao 2-2 dhidi ya Arsenal katika Uwanja wa Emirates katika mchezo uliokuwa wa kuvutia. City ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ndio walioanza kufunga bao la kuongoza kupitia kwa Sergio Aguero katika dakika ya 28 aliyemalizia pasi murua ya Jesus Navas kabla ya Jack Wilshere hajasawazisha bao hilo katika dakika ya 63 kwa juhudi binafsi. Arsenal hawakuishia hapo kwani walipambana na kuhakikisha wanapata bao la pili kupitia kwa Alex Sanchez katika dakika ya 74 lakini Demicheles aliharibu sherehe baada ya kusawazisha katika dakika ya 84. Kwa matokeo hayo Arsenal sasa imevuna alama sita katika michezo minne waliyocheza huku City wao wakivuna alama saba katika michezo minne walioyocheza.


No comments:

Post a Comment