KOCHA wa timu ya taifa ya Uingereza, Roy Hodgson amesema wapinzani timu yake katika mechi za kufuzu michuano ya Ulaya mwakani hawawezi kuwavutia mashabiki wengi kwenda kuwaangalia katika Uwanja wa Wembley. Mashabiki 40,181 pekee ndio waliotizama mchezo wa jana wa kirafiki ambao Uingereza ilishinda kwa bao 1-0 dhidi ya Norway ikiwa ni kiwango cha chini kabisa toka Uwanja wa Wembley ufunguliwe tena mwaka 2007. Uingereza inatarajiwa kucheza na San Marino, Estonia, Switzerland, Slovenia na Lithuania katika mechi zake za kufuzu michuano hiyo katika uwanja huo wa Wembley. Akihojiwa Hodgson amesema itakuwa kazi ngumu kuwashawishi mashabiki kwasababu wapinzani wanaocheza nao hawatawavutia. Mchezo wa jana ulikuwa wa kwanza kwa Uingereza toka walipong’olewa katika hatua ya makundi kwenye Kombe la Dunia baada ya kutandikwa na Italia na Uruguay huku wakitoa sare na Costa Rica.
No comments:
Post a Comment