Monday, September 22, 2014

MESSI ZAIDI YA RONALDO - ZAMBROTTA.

BEKI wa zamani wa vilabu vya Juventus, AC Milan na Barcelona Gianluca Zambrotta amesema wote Lionel Messi na Cristiano Ronaldo ni wachezaji wa kipekee lakini anaamini Messi ambaye walicheza wote akiwa Barcelona ana kipaji cha ziada kuliko Ronaldo. Zambrotta ambaye amecheza misimu miwili Barcelona kuanzia mwaka 2006 mpaka 2008 amekiri kufahamu mara moja kuwa Messi ana kipaji cha kipekee. Zambrotta amesema alipofika Barcelona mwaka 2006 Messi alikuwa bado mdogo lakini kipaji chake kilikuwa kinajionyesha wazi kwani alikuwa mtu wa kawaida nje ya uwanja lakini pindi aingiapo ndani anabadilika na kuwa mtu mwenye ufanisi wa hali ya juu. Nyota huyo wa zamani aliendelea kudai kuwa pamoja na kwamba wote wana uwezo sawa katika kufunga mabao lakini kwa mawazo bado anadhani Messi ana vitu vua ziada ambavyo vinaweza kubadilisha mchezo wakati wowote kuliko ilivyo kwa Ronaldo.

No comments:

Post a Comment