Monday, September 22, 2014

BALOTELLI AZUA JAMBO TWITTER KUFUTIA KIPIGI CHA MAN UNITED.


POLISI nchini Uingereza wameanzisha uchunguzi kuhusu tukio ambalo mshambualiji wa klabu ya Liverpool na timu ya taifa ya Italia Mario Balotelli alitukanwa kutokana na rangi ya ngozi yake kupitia kwa mtandao wa kijamii wa Twitter. Polisi katika mji wa Merseyside wameanzisha uchunguzi kufuatia matusi hayo yaliyotokea baada ya nyota huyo kutuma ujumbe akicheka kichapo cha Manchester United walichpata kutoka kwa timu ndogo ya Leicester City jana. Balotelli aliandika ujumbe huo ambao ulisambazwa kwa zaidi ya 150,000 kwa mashabiki wake. Hata hivyo miongoni mwa wale waliouona ujumbe huo walimshambulia kwa kucheka kichapo hicho cha United na wengine kufikia hatua ya kumtukana kwa misingi ya rangi yake. Pamoja na Uraia wa Italia alionao, Balotelli mwenye umri wa miaka 24 ana asili ya Afrika. Polisi tayari wamefunga kurasa kadha zilizotuma ujumbe huo huku wakianza uchunguzi waliozimiliki ni kina nani na wanaishi wapi iliwakamatwe na kujibu mashataka ya ubaguzi wa rangi. Kundi linalopigania kumaliza ubaguzi wa rangi katika michezo Kick It Out lilisema kuwa baada ya kuarifiwa kuwepo kwa matusi yenye kumdhalilisha Balotelli, kundi hilo lilianzisha uchunguzi kwa ushirikiano na polisi wa mitandao ya kijamii.

No comments:

Post a Comment