Wednesday, September 24, 2014

MILNER ATAKA UHAKIKA WA NAMBA KABLA YA KUSAINI MKATABA MPYA.

KIUNGO wa Manchester City, James Milner amekiri kuwa anataka uhakika kwa namba katika kikosi cha kwanza kabla ya kuamua kuongeza mkataba mwingine katika klabu hiyo zaidi ya msimu huu. Milner anamaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu na wakati City wakihaha kuhakikisha wanamuongeza mkataba mwingine, nyota huyo wa kimataifa wa Uingereza hana na suala hilo kwasasa. Baada ya kuachwa katika benchi katika mechi tatu za Ligi Kuu za mwanzo za City, Milner mwenye umri wa miaka 28 alianza katika michezo iliyofuatia ya ligi dhidi ya Arsenal na Chelsea. Milner mwenyewe amesema anataka kuangalia mambo yanavyokwenda kwanza kabla ya kukubali mkataba mpya huku suala la kuanza katika kikosi cha kwanza likiwa jambo la kwanza katika akili yake. Milner aliendelea kudai kuwa anajua amebakisha mwaka mmoja katika mkataba wake na tayari ameshazungumza na klabu na anapenda kubakia hapo ila jambo la kwanza kama mchezaji anahitaji kucheza mara kwa mara.

No comments:

Post a Comment