Wednesday, September 24, 2014

ALGERIA SASA YAJITOSA KUWANIA AFCON 2017.

BAADA ya kukosa nafasi ya uandazi wa michuano ya Mataifa ya Afrika-AFCON mwaka 2019, 2021 na 2023, Shirikisho la Soka la Algeria sasa limetangaza kutuma maombi ya kutaka uenyeji wa michuano hiyo mwaka 2017. Taifa hilo lililopo kaskazini mwa bara la Afrika litachuana na nchi za Ethiopia, Ghana, Kenya, Tanzania, Mozambique, Zimbabwe na Misri katika kugombea nafasi hiyo. Libya ilishindwa kuandaa michuano hiyo kufuatia vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoendelea nchini humo toka kuondolewa kwa utawala wa Muamar Gaddafi. Mshindi katika kinyang’anyiro hicho anatarajiwa kutangazwa mapema mwakani na Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF. Cameroon wao walishinda haki za kuandaa michuano hiyo mwaka 2019 wakati Ivory Coast na Guinea wao walipata nafasi ya kuandaa michuano ya mwaka 2021 na 2023.

No comments:

Post a Comment