Wednesday, September 24, 2014

KLOPP AUNGANA NA GUARDIOLA KUTETEA AFYA ZA WACHEZAJI KUTOKANA NA RATIBA NGUMU ZA MECHI.

MENEJA wa klabu ya Borussia Dortmund, Jurgen Klopp amemuunga mkono Pep Guardiola kwa kauli yake kuwa ratiba ya mechi nyingi inaumiza afya za wachezaji. Guardiola ambaye anainoa Bayern Munich alilalamika kuwa ratiba iliyobana katika soka la wakati huu linawaumiza sana wachezaji na Klopp sasa ameonya kuwa wachezaji watalazimika kustaafu soka mapema pindi wafikishapo miaka 30 kama hali hiyo haitabadilika. Klopp amekaririwa akidai kuwa katika kipindi cha miaka 10 inayokuja kutakuwa hakuna wachezaji wanaoweza kucheza mpaka kufikia umri wa miaka 35. Klopp amesema wachezaji wa zamani walioshika nafasi muhimu katika uongozi wameshasahau jinsi mambo yalivyokuwa magumu wakati wakicheza soka. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa michuano ya Ulaya mwakani itakuwa na timu 24 kwasababu baadhi ya watu wanaona ni wazo zuri lakini wanasahau kuwa wanawaumiza wachezaji kwa kuwachezesha mechi nyingi zaidi.

No comments:

Post a Comment