Wednesday, September 24, 2014

LA GALAXY YATHIBITISHA KUMTAKA PIRLO.

KIUNGO mahiri wa kimataifa wa Italia, Andrea Pirlo anatarajiwa kufanya uhamisho wa kushtukiza kwenda klabu ya Los Angeles Galaxy ya Marekani. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 35 ambaye kwasasa anakipiga katika klabu ya Juventus amecheza soka nchini Italia katika muda wake wote lakini pamoja na kupewa mkataba wa miaka zaidi galaxy wanafikiria kumsajili nyota huyo. Klabu hiyo ya zamani ya David Beckham inamtaka kiungo huyo mkongwe kuziba nafasi ya London Donovan ambaye ametangaza kustaafu soka mwishoni mwa msimu wa Ligi Kuu ya Soka nchini Marekani-MLS baadae mwaka huu. Mwezi uliopita Pirlo alikaririwa akidai kuwa hana sababu ya kuhama kwani anaona maisha bado mazuri Juventus na kuongeza kuwa labda baada ya miaka miwili ya mkataba wake kunalizika anaweza kufikiria kwenda Marekani. Hata hivyo muda huo unawezekana usifike kwani kocha wa Galaxy Bruce Arena tayari amethibitisha nia yao ya kumsajili mkongwe huyo.

No comments:

Post a Comment