MENEJA wa klabu ya Chelsea, Jose Mpourinho amedai kuwa hana tatizo na kikosi chake kujipa motisha wenyewe kabla ya kuivaa Manchester City Jumapili katika mchezo wa Ligi Kuu utakaochezwa katika Uwanja wa Etihad. Meneja huyo raia wa Ureno ameshuhudia kikosi chake kikishinda kila mchezo wa Ligi Kuu msimu huu lakini waligonga mwamba kwa Schalke Jumatano wakati walipolazimishwa sare. Hata hivyo, Mourinho anaamini Chelsea ina uwezo wa kuwafunga mahasimu wao hao katika mbio za ubingwa na kusisitiza wanajiamini kwa uwezo wao kuelekea katika mchezo huo. Mourinho mwenye umri wa miaka 51 amesema siku zote ni jambo zuri kucheza dhidi ya timu kubwa kwani inafanya kazi yake kuwa rahisi. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa wanaiheshimu City kwasababu wanastahili lakini wao pia wanajiamini kufanya vyema katika mchezo huo.
No comments:
Post a Comment