Saturday, September 20, 2014

LIGI KUU TANZANIA BARA KUANZA RASMI LEO.

LIGI Kuu Tanzania bara inaanza kutimua vumbi rasmi leo kwa viwanja mbalimbali nchini vikitarajiwa kuwaka moto katika mechi za ufunguzi huku mashabiki wakiwa na hamu kubwa ya kuona jinsi timu zilivyojiandaa kwa ajili ya msimu mpya. Kwa upande wa Dar es Salaam leo mabingwa watetezi Azam FC wao wataanza kampeni zao kwa kuikaribisha Polisi ya Morogoro katika Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi huku wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa Ngao ya Jamii kwa Yanga. Yanga mabingwa wa Ngao na washindi wa pili wa ligi msimu uliopita wao watakuwa na kibarua kizito pale watawavaa wakata miwa wa Mtibwa Sugar Jamhuri mkoano Morogoro, wakati Mbeya City washindi wa tatu wa ligi wao wakianzia nyumbani katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine kwa kuikaribisha JKT Ruvu. Timu za Stand United ya Shinyanga na Ndanda FC ya Mtwara ambazo zote zimepanda daraja msimu huu nazo zitakuwa dimbani kuonyeshana kazi katika Uwanja wa Kambarage, Mgambo JKT watakuwa wenyeji wa Kagera Sugar katika Uwanja wa Mkwakwani huku Ruvu Shooting wakiwakaribisha Tanzania Prison katika Uwanja wa Mabatini.

No comments:

Post a Comment