Saturday, September 20, 2014

SAMATTA, ULIMWENGU KIBARUANI LEO.

WASHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu leo watakuwa na kibarua kizito pale klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC itakapomenyana na Entene Setif ya Algeria. Mchezo huo wa nusu fainali ya mkondo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika itachezwa katika Uwanja wa Setif maarufu kwa jina la Mei 8, 1945. Hii itakuwa mara ya pili kwa timu hizo kukutana ambapo mara ya kwanza ilikuwa katika mechi za hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho ambapo Mazembe walifanikiwa kutoa sare ya bao 1-1 katika mchezo wa mkondo wa kwanza huku wakiwatandika Setif kwa mabao 4-2 katika mchezo wa marudiano uliochezwa jijini Lubumbashi. Setif ilishindwa kufurukuta katika kundi B walilokuwepo baada ya kuburuza mkia, wakati Mazembe waisonga mbele mpaka hatua ya nusu fainali mpaka fainali na baadae kuja kufungwa na CS Sfaxien ya Tunisia kwa jumla ya bao 1-0 na kuibuka bingwa wa michuano hiyo. Mchezo mwingine wa nusu fainali unatarajiwa kuchezwa kesho jijini Kinshasa ambapo AS Vita watakuwa wenyeji wa Sfaxien.

No comments:

Post a Comment